KUHUSU SISI (ABOUT US).

ABOUT US (KUHUSU SISI)


UTAMBULISHO WA MATUMAINI GROUP.

UTAMBULISHO WA MATUMAINI GROUP.

Matumaini group ilianzishwa mwaka 2008 na kupata usajili mwaka uliofuata january 3,2009 Wizara ya mambo ya ndani.Namba ya usajili ni SA.16166.

1.2) MAONO YA MATUMAINI GROUP (VISION)
Kuwa na jamii yenye wanawake na wanaume,vijana na watoto wenye matumaini na uwezo wa maisha yao katika kiwango chenye mafanikio kiuchumi,kijamii na kiutamaduni.


1.3) KUSUDIO LA KUANZISHWA KWA MATUMAINI GROUP MISSION
Kuweza jamii katika nyanja za uchumi,kijamii na kielimu ili kuleta mabadiliko endelevu katika maisha ya makundi ya watu katika jamii.

kufanya utetezi wa makundi yanayo nyanjasika kupitia mifumo,kuongeza uelewa katika umma na zisizo za umma.


1.4) MSINGI WA IMANI YETU KATIKA MAONO.
Tunathamini watu.Uwajibikaji na uwazi.Kufanya kazi kwa ubora,kuzalisha matunda yenye manufaa kwa jamii.

 UTETEZI NA SERA
ELIMU:
Kupata uelewa na ufahamu katika jamii juu ya haki za makundi mbalimbali.kwa mfano wanawake na watoto.
 
Uhamasishaji:
Kuwa na makundi yanayohamasika yaliyopata ujuzi na utetezi na kuanzisha jitihada za kuhudhuria kwenye vikao ambavyo wanawake na wanaume watasemea haki zao,kuanzia ngazi ya mtaa na kata wilayani hadi taifa.

Serikali za Mitaa na kata:.
Kutafuta habari kutoka kwa serikali hizo na kuzifanyia kazi kuwaona viongozi ambao wanao uwezo wa kufanya maamuzi na kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii wanayoitumikia.

Shabaha na Malengo:
  • Kufanya utetezi na kuwa na sera endelezi.
  • kuwajengea uwezo wanawake,wanaume,vijana,wasichana na watoto.
  • Kujenga uwezo wa kufanya biashara na eimu ya ujasiliamali kwa kutumia vitu vinavyowazunguka.
  • kujenga mahusiano na vyombo vinavyosaidia jamii katika kuboresha kipato kama vile taasisi na mashirika.
1.5) ENEO LA KUFANYIA KAZI.
Kikundi cha matumaini kinafanyia kazi maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es salaam kwa sasa na baadaye kusambaza huduma hii nchi

1.6) AINA YA VIKUNDI.
Kikundi hiki si cha kiserikali.Kina wanachama wa kujitolea na hakifungamani na chama chochote cha kisiasa wala dini.kikundi hiki hakijiendeshi kwa faida bali kwa kuihudumia jamii.

1.7) KAZI ZA MATUMAINI GROUP:
  • Tunatoa huduma ya wagonjwa majumbani HBC,Ushauri nasaha na huduma shufaa.
  • Tunahudumia watoto yatima
  • Elimu ya afya ya uzazi kwa vijana na kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya.
  • Tunapambana na uharibifu wa mazingira.
  • Tunatoa Elimu ya kupambana na maambukizi zidi ya VVU/UKIMWI
  • Tunahamasisha upimaji wa VVU kwa hiari
  • Tunapambana na vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake vinavyosababishwa na wanaume wasio na maadili.
  • Tunatoa elimu ya maswala ya kijinsia
  • Tunatoa warsha za kivuko (stepping stone)kwa vijana na jamii kiujumla.
Hakuna maoni:

0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More