Jumatatu, 1 Septemba 2014

UJIO WA UGENI WA TACAIDS – MATUMAININ GROUP 19/06/2014


LENGO KUU: - TATHMINI YA SHUGHULI ZA UKIMWI ZINAZOFANYWA NA ASASI KATIKA MANISPAA



Matumaini Group ilianzishwa mwaka 2008 na kupata usajili Januari 3, 2009 Wizara ya Mambo ya ndani kwa namba ya usajili SA. 16166.

MATUMAINI Group ilitembelewa na Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI TANZANIA (TACAIDS) mnamo tarehe tajwa hapo juu, ikiwa katika kiufanya tathmini ya asasi zinazofanya shughuli za UKIMWI katika Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar Es Salaam.

MAONO YA MATUMAINI (VISION)

Kuwa na jamii yenye wanawake na wanaume, vijana na watoto wenye matumaini na uwezo wa maisha yao katika kiwango chenye mafanikio kiuchumi, jamii na kiutamaduni



MATUMAINI group imekuwa mstari wa mbele katika kuihudumia jamii hasa watoto na vijana wenye umri kati ya miaka 10 – 24 na jamii kwa ujumla juu VVU na UKIMWI.

MATUMAINI GROUP inafanya kazi kwa karibu na uongozi wa serikali ya mtaa, kata, Manispaa ya Kinondoni. Na kwa ushirikiano huo tumeweza kufikia mafanikio yafuatayo:-



a) Wageni kutoka TACAIDS na Manispaa

Katika kutembelewa na ugeni huo mambo mengi yalifanyika yakiwemo: Uzinduzi wa kipeperushi cha MATUMAINI group kinachotuelezea, tumetoa huduma ya upimaji wa VVU na ushauri nasihi samabamba na utoaji wa elimu ya afya ya uzazi na VVU/UKIMWI kwa vijana.

I) Miongoni mwa wageni waliokuja ni:-

Moris Lekule (TACAIDS), Songoro Mnyonge naibu MEYA kinondoni, Samuel Mhando M/CMAC Kinondoni vijana, Dr. Ackim Mwaikasi ofisi ya RS/RMO, Dr. Samuel Lema ofisi ya DMO
Naibu meya manispaa ya kinondoni akipongeza wanaMATUMAINI kwa kazi wanazo fanya sambamba na taarifa wanazozipata kuwa ni zakuigwa baada ya kusomwa kwa taarifa ya MATUMAINI GROUP









ii) Viongozi wa mtaa na kata


Mwenyekiti wa mtaa sinza A Juma Mgenwa,Manyaga Magreth, W. Mhina (mjumbe sinza A), Raymond Kaminyage, Ibrahimu A. Mabewa MEO Sinza A, Ally R. Mgaya (mjumbe s/mtaa), Silvan Kiwale Photoana, Magreth Mtawali, Pili Hamisi (mjumbe serikali ya mtaa), Teresia S. Chihota (MWANACHI Communication)



1: Tathmini kwa MATUMAINI Group


Mara baada ya kuwasili na kusaini kitabu cha wageni, taarifaa ya MATUMAINI group ilisomwa iliyozungumzia kazi, mafanikio, changamoto na mipango ya baadae, na kati ya yote ifuatayo ni muhtasri wa taarifa hiyo:





Mafanikio
UMRI
WASIO NA VVU/UKIMWI
WENYE VVU/UKIMWI

ME
KE
JUMLA
ME
KE
JUMLA
14
0
0
0
0
0
0
15 – 24
2991
1860
4851
0
6
6
25 – 34
3792
3540
7332
8
6
14
35 – 49
182
108
290
6
2
8
50+
45
13
58
0
4
4

7010
5521
12531
14
18
32






i) Changamoto

· Kujitoa kwa wanachama kutokana na kuzidi kwa michango ya ndani ya asasi

· Ugumu wa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutokomeza UKIMWI na VVU

· Gharama za uendeshaji ofisi ikiwemo pango na vitendea kazi vingine.



i) Mipango ya baadae

· Kuendelea kushirikiana na viongozi wa mtaa, kata na Manispaa katika kuiokoa jamii na janga la UKIMWI

· Kuendelha mikutano na majadiliano yatakayojumuisha vijana, wazazi, viongozi wa serikali, waalimu, viongozi wa dini, watu mashuhuri n.k ili ujumbe uweze kuenea kwa haraka zaidi.

· Kutumia klabu ya vijana katika kikamilifu ili wawafundishe vijana wenzao juu ya UKIMWI na VVU

· Kuendelea kutoa elimu katika shule za msingi, sekondari, vyuo na katika mikusanyiko mikubwa ya watu.

· Kuendesha zoezi la ufuatiliaji kupima viashiriria, matokeo na matarajio.

· Kuendelea kufanya mchakato wa upatikanaji wa fedha kutoka kwa wafadhili mbalimbali wanaofanya shughuli sawa na MATUMAINI.

· Kuandaa, kutunza na kutuma taarifa ngazi ya kata na Manispaa



2: Uzinduzi wa Kipeperushi

Mheshimiwa kaimu mkurugenzi wa TACAIDS aliweza kukizindua ramsi Jumla ya vipeperushi vilivyozinduliwa ni 6324
kaimu mwenyekiti wa tume ya kuthibiti ukimwi( TACAIDS) akifungua boksi lenye kipeperushi cha MATUMAINI group, katika ugeni wa kiofisi sambamba na uzinduzi wa kipeperushi hicho iliyofanyika katika viwanja vya nje ya ofisi ya MATUMAINI group

Kaimu mwenyekiti wa tume ya kuthibi ukimwi TACAIDS akizindua rasmi kipeperushi cha MATUMAINI

Makamu mwenyekiti wa TACAIDS akitoa hotuba baada ya uzinduzi wa kipeperushi cha matumaini 

(Baadhi ya viongozi WA TACAIDS Na Manispaa wakiendela kujifunza kutoka katika vipeperushi mbalimbali juu ya afya ya uzazi, virusi vya VVU na UKIMWI

 3. UPIMAJI WA VVU
UMRI
ME
KE
JUMLA
0 – 24
19
32
51
25 – 34
11
8
19
35 – 49
7
4
11
50 -
4
9
13
JUMLA
41
53
94




4: Elimu ya afya ya uzazi na ukimwi kwa vijana


· Vijana wapatao 60 wenye umri chini ya miaka 24 walipatiwa mafunzo

· Vijana wakike wenye umri wa miaka chini ya miaka 24 walikuwa 37

· Vijana wakiume wenye umri wa miaka chini ya miaka 24 walikuwa23

· Vijana wenye umri wa miaka 25 -35 wakike walikuwa 21 Vijana wenye umriwa miaka 25-35 wakiume walikuwa 11
Baadhi ya vijana wakisikiliza kwa makini kutoka kwa waelimishaji rika wa MATUMAINI group somo juu ya haki ya afya uzazi kwao sambamba na majukumu yao kama vijana katika jamii zao  


Mada zilizofundishwa

  • · Vijana na ukimwi
  • · Haki ya afya ya uzazi
  • · Magonjwa ya ngono
  • · Wajibu wa kijana juu ya afya ya uzazi
  • · Umuhimu wa kupata huduma na kutafuta taarifa zinazo husu afya ya uzazi kwa vijana
  • · Stadi za maisha


  

Picha ya pamoja na vijana baada ya kutembelewa na viongozi –tume ya kuthibiti UKIMWI (TACAIDS)



NENO LA SHKRANI


MATUMAINI group inatoa shukrani za pekee kwa serikali ya mtaa wa Sinza “A” na kata ya Sinza. Pili shukrani ziende kwa Manispaa ya Kinondoni. Tatu kwa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI wote kwa pamoja kwa kutambua mchango na nafasi ya MATUMAINI group katika wilaya ya Kinondoni. Na mwisho tunapenda kuwashukuru vijana wenyewe ambao ndio wadau wakuu, wazazi, walimu na jamii kwa ujumla katika kutimiza lengo moja la jamii yenye usawa bila kujali tofauti za kafya au kipato.


0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More